Nembo ya RE/MAX

Ukiwa Na RE/MAX unachagua njia sahihi.

Wateja wana haja zinazofanana: ni mahali wanapopaita nyumbani. Wao wanahitaji ushauri wa kitaalamu katika kuwaongoza kwa maswala ya kununua nyumba mpya au kuuza mali yao. Katika jamii yoyote duniani kote , kwa wakati wowote , mamia ya shughuli za uuzaji nyumba na mashamba uhudumiwa na maajenti.

Hata hivyo, kuna pia asilimia kubwa ya shughuli za uuzaji nyumba na mashamba ambazo hufanyika bila ya kuutafuta ushauri wa wataalamu wenye ujuzi. Jambo hili hutokea kwa sababu wateja kujisikia uwiano kati ya huduma ya wanayopokea na gharama wanayotozwa haziambatani. Wakati huo huo, katika RE/MAX , uwiano huu ni mojawapo ya bora zaidi kote duniani.

Wakati shugli zinakaba maisha ya watu, maajenti wetu huzidi kuwasiliana mara kwa mara na wateja wao wa zamani na kuendelea kutumikia mahitaji yao maalum. Maajenti wetu hujenga wateja wa maisha . Wao pia wanaweza kupata nafasi murwa kwako kwani wanajua masoko yao ya nyumba na mashamba vyema.

Usawa wa Nembo

RE/MAX inatoa mikakati mbali mbali ya Nembo zake – utangazaji kwenye vyombo vya habari unawezesha na kuhakikisha kutambuliwa duniani kote kwa nembo ya RE/MAX ilhali utangazaji wa kibinafsi unaipa ofisi uwepo katika soko. Mbinu kabambe za utangazaji zinazokidhi mahitaji ya soko la Kenya zitakuwa muhimu katika kila hatua.

Jinsi tunavyotambulika

"Puto " huwa mwitikio wa kwanza unapowauliza maajenti au wamiliki ju ya uhusiano wao na RE/MAX. "Bila shaka, kuna baadhi ya mambo mengine, lakini puto iko kila mahali. Wateja hujua wewe ni nani bila ya wewe kuwaeleza ". Hakika Puto inaashiria kikamilifu mawazo ya RE/MAX ya uvumbuzi na uongozi , ikionyesha dhana ya kuwa huru - katika biashara kwa ajili yako mwenyewe, ukielekezwa na nembo yenye umaarufu duniani kote bali sin a wewe mwenyewe.

Hakuna Anayeuza Nyumba na mashamba zaidi kuliko RE/MAX

Hili ni jambo ambalo tunaweza kujigamba nalo. Lakini kuna zaidi ya hayo : kauli hii ni mojawapo ya zingine nyingi ambazo maajwnti na wamiliki wanaweza kujivunia wakiwa katika RE/MAX. RE/MAX imesajili kauli mbalimbali ya itikadi zake, hivyo basi kutambulika na wateja wote kote ulimwenguni.

Kujiendeleza kibinafsi

Kujikuza mwenyewe ni sehemu ya uhuru unaopata katika RE/MAX. Njia bunifu za kujitangaza na kujiendeleza huwa zinapewa nguvu  na hakuna vikwazo. Kanuni tu ni kufuata nembo halisi zilizotengwa na kuambatana na mwongozo wa RE/MAX.

Kutambua wateja

Ni nani haswa anayeweza kujua vyema jinsi ya kufikia wateja watarajiwa katika kila sehemu kuliko Maajenti na wamiliki wenyewe? Hakuna. RE/MAX inakuwezesha kuchagua njia yako ya matangazo – yaani, unajua bora ni vyombo vipi vya habari vitakavyo fanikisha na kuunga mkono utetezi wako! Hii ni hali ambayo huwezesha ushidi kupatikana kila upande kwani wateja wakijitambulisha na wewe wanajitambulisha na RE/MAX. Jambi hili hukuza uaminifu baiba yako na hao na huchangia pakubwa katika kuleta biashara Zaidi kwako.