1. Timu yenye uzalishaji zaidi katika uuzaji nyumba na mashamba : Hakuna yeyote anayeuza nyumba na mashamna duniani kuliko RE/MAX. Ukiungwa mkono na mafunzo bora , zana bora katika biashara na nguvu za jina la RE/MAX katika uuzaji nyumba na mashamba, ni rahisi mno kufanya biashara. Mbona basi uchague kazi mahala pengine ilhali unaweza kujiunga na shirika/kampuni bora zaidi duniani?
2. Gundua tofauti ya RE/MAX:
Falsafa inayolenga maajenti.
Dhana ya malipo ya juu zaidi – unaweka kiwango kikubwa cha pesa unazoleta.
Kutambuliwa kwa nembo ya RE/MAX katika setka ya uuzaji nyumba na mashamba.
Teknolojia ya Kisasa na Mafunzo.
Mazingara yanayokuwezesha kukua.
Mtandao mkubwa wa kupata msaada.
Kupata rufaa bila malipo zaidi.
Huduma bora na ya kufana zaidi.
Unadhibiti biashara yako wewe binafsi.
Hizi ni baadhi tu ya sababu za kwa nini maajenti wa RE/MAX huwazidi ujuzi wengine katika sekta hii.
3. Kuchanganya nguvu yako na yetu : RE/MAX inatoa mafunzo, zana, na msaada katika kuongeza mauzo yako. Wakati huo huo , wewe hubakia kudhibiti na kufurahia uhuru wa kuendesha biashara yako kwa njia unayotaka. RE/MAX inakupa nafasi murwa na hukuwezesha kukua hadi unapotarajia kwa urahisi.
4. Jifunze zaidi ili ulipwe zaidi : Kupitia RE/MAX University pokea elimu na mafunzo kutoka kwa wataalam wa sekta. Zaidi ya kanda za video 1,100 video na masomo kwenye mtandao zinapatikana kwa masaa 24 kila siku kokote ulipo hata kupitia tarakilishi na simu za mkononi. Hata iwe habari, masomo au hata motisha, yote haya utayapata katika RE/MAX University na utayaona matokeo.
5. Pata mafunzo na ujenge uhusiano katika kongamano zetu za kimataifa : milango ya kukua hufunguka wazi wakati unapohudhuria kongamano za RE/MAX za kiimataifa ya Misri , Marekani au nchi nyingine yoyote. Mikutano hii huwa fursa za kujifunza , kubadilishana mawazo , kutangaza nyumba ulizo nazo kwa sasa, kutambuliwa kwa mafanikio yako na kujenga mtandao na maajenti wenzao duniani.
6. Wateja zaidi kutoka maeneo zaidi : Hata uwe wapi diniani, wateja wanaweza kukupata punde tu wanapofika katika tovuti ya remax.com pamoja na global.remax.com . Hizi ndio tovuti zinazotembelewa zaidi duniani kwa maswala ya uuzaji nyumba na mashamba kila mwezi.
7. Katika huduma yako : teknolojia, zana na msaada : RE/MAX bado iko mstari wa mbele katika teknolojia, pamoja na zana za kisasa na mifumo ya msaada kwa maajenti. Na yote haya yameundwa ili kusaidia biashara yako iwe na mapato zaidi.
8. Fanya biashara yako itambe kote duniani: Wakati unapojiunga na RE/MAX , unakuwa mojawapo ya mguvu ya mauzo ya zaidi ya maajenti 93,000 katika nchi zaidi ya 90 . Unapata manufaa ya mtandao wa rufaa ili kupata ufanisi zaidi.